Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa
huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watoto 32, walimu 2 na
dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha, vilivyosababishwa na
ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu -
Arusha.
Tunasikitika sana kwa kuwa ajali hii
imetokea wakati wazazi, walezi na walimu wakitekeleza wajibu wao wa
msingi wa kumpatia mtoto haki ya kuendelezwa Kielimu.
Kufuatia
msiba huu mkubwa, kwa niaba ya Wizara na kwa niaba yangu mwenyewe
ninatoa pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na
Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa
wanaandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali.
Tunamuomba .
Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira
katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia
za marehemu na Taifa kwa ujumla.
Tunaziombea
roho za watoto wetu wapendwa zipumzishwe mahali pema peponi, Amiin. Ni
maombi yetu pia kuwa Majeruhi waliopo hospitalini watapata nafuu ili
waweze kuendelea na masomo.
Ummy Mwalimu, Mb
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/05/2017
SHARE
No comments:
Post a Comment