Taasisi
ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE)
inayojishughulisha na masuala ya watu wenye Ualbino yenye makao makuu
yake nchini Uholanzi leo imetoa elimu kuhusu mambo ya ualbino kwa
viongozi Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
(DKMZV).
Taasisi hiyo imetoa elimu hiyo leo Ijumaa May 25,2017 na Mwenyekiti wa
JTFE, Pieter Staadegaard kutoka nchini Uholanzi na Mkurugenzi wa Idara
ya Ushawishi na Utetezi kutoka JTFE Josephat Torner anayeishi nchini
Tanzania wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi Kusini
Mashariki ya Ziwa Victoria kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano
kanisa la KKKT Ebenezer kanisa kuu Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hicho,Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya
Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard alisema
lengo la taasisi hiyo kushughulika na mambo mbalimbali yanayohusu watu
wenye ualbino ndani na nje ya Tanzania.
Staadegaard ambaye anaishi na mtoto mwenye ualbino alitumia fursa hiyo
kuwaomba viongozi wa dini kushiriki kikamilifu katika kutokomeza vitendo
vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye ualbino kwani ni vitendo ambayo
vinamchukiza hata mwenyezi mungu.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka JTFE Josephat
Torner alisema kutokana na vitendo wanavyofanyiwa watu wenye
ualbino,vita hiyo inatakiwa kumalizwa kiimani kwani mambo ya kishirikina
hayawezi kumalizwa kwa mitutu ya bunduki bali watu kubadilika kifikra.
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala alisema kanisa hilo liko
mstari wa mbele katika kupiga vita ukatili wanaofanyiwa watu wenye
ualbino na tayari walishaunda idara maalum kwa ajili ya kushughulikia
masuala hayo.
Nimekuwekea picha za matukio hapa chini
Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi
ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat
Torner akimtambulisha Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat
Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard (kushoto) kwa Askofu
wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria -Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza katika kikao hicho
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akizungumza kwa lugha ya Kiingereza huku
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa
ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akitafsiri
kwa lugha ya Kiswahili
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa
ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akisisitiza
jambo
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa
ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akielezea
umuhimu wa viongozi wa dini kushiriki katika vita dhidi ya ukatili
wanaofanyiwa watu wenye ualbino
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu
ya Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala akizungumza.Kushoto ni Katibu Mkuu wa kanisa
hilo Daniel Mono,Kulia ni Msaidizi wa Askofu kanisa hilo,Trafaina Nkya
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala akizungumza jinsi kanisa hilo linaendelea na
vita dhidi ya vitendo dhidi ya watu wenye ualbino
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza
Wajumbe wakifurahia jambo
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala alisema kanisa hilo limekuwa mstari wa mbele
katika vitendo vya kupiga vita ukatili dhidi ya watu wenye ualbino
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe
(JTFE) Pieter Staadegaard akiagana na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi
Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa
ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akiagana na
Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt.
Emmanuel Joseph Makala
Mkurugenzi wa Idara ya Ushawishi na Utetezi kutoka Taasisi ya Kimataifa
ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Josephat Torner akiagana na
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria,Trafaina Nkya
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa ya Josephat Torner Foundation Europe (JTFE) Pieter Staadegaard akiagana na Katibu Mkuu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Daniel Mono.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment