Timu ya mpira wa
miguu ya Tanzania inatarajiwa kuanza mazoezi yake usiku huu baada ya
kufika salama mjini Alexandria,nchi Misri kwa ajili ya kuweka kambi.
"Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku nyingine nitafanya asubuhi na jioni."
Taifa Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi 'L' ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment