Shabiki
mmoja amefariki dunia katika ajali ya gari katika eneo la Dumila mkoani
Morogoro, ndani ya gari hilo alikuwamo nahodha wa Simba, Jonas Mkude.
Mkude
ni kati ya majeruhi na wengine watatu pia wameumia na tayari wako
njiani wakitoka Dumila kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Muslah Al Rawah amethibitishwa kwa majeruhi hao kupelekwa Morogoro.
Mkude
alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba
kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la
Shirikisho.
Mkude alikuwa katika gari na baadhi ya mashabiki wa Simba na gari lilipasuka tairi na kuanguka. Mtu mmoja amefariki dunia.
SHARE
No comments:
Post a Comment