TRA

TRA

Saturday, May 20, 2017

Wachimbaji wadogo wa madini, wachuuzi na madalali nchini kufanya mdahalo wa kitaifa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


wad1
Viongozi wa chama cha wachimbaji madini Mkoani Manyara, Marema Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro, wakizungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita
wad2
Mtafiti wa shirika la IIED la Uingereza, Fitsum Weldegiorgis akizungumza juzi na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara, Marema (kushoto) ni Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini, Amani Mhinda.
wad3
Viongozi wa chama cha wanunuzi na wachuuzi wa madini ya Tanzanite Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuzungumza na viongozi wa shirika la Haki Madini juu ya mdahalo wa kitaifa wa madini unaotarajia kufanyika Mkoani Geita.
……………………………………………………………………….
Wachimbaji wadogo wa madini, wachuuzi na madalali wa madini nchini wanatarajia kufanya mdahalo wa kitaifa juu ya umuhimu wa sekta ya madini na namna ya kuwanufaisha zaidi.
Mkurugenzi wa shirika la Haki Madini Amani Mhinda, akizungumza mji mdogo wa Mirerani na viongozi wa chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema) alisema mdahalo huo utafanyika mkoani Geita.
Mhinda alisema lengo la mdahalo huo ni kuwaleta wadau mbalimbali kwa pamoja ili kuzungumzia changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa wachimbaji wadogo na kutafakari kitaifa maono ya wachimbaji.  
Alisema wanatarajia kufanya mdahalo huo mwishoni mwa mwezi Juni kwa kushirikiana na shirika kiongozi duniani la maendeleo la International Institute for Environment and Development (IIED).
“Haki madini tunarajia mpango huu utatoa jukwa hitajika kwa wadau kushirikiana na kubadilishana ujuzi na kukuza utawala bora kuwa sauti kubwa, usalama na utengenezaji,” alisema Mhinda.
Alisema uchimbaji mdogo wa madini unaweza kutoa mchango chanya wenye umoja na usawa wa maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi, kwani husaidia mamilioni ya watu hasa wanawake na watoto.
Katibu wa Marema Tawi la Mirerani, Abubakari Madiwa alisema kupitia mdahalo huo wanatarajia wachimbaji mdogo kunufaika kwa kujengewa uwezo hivyo wamejiandaa kushiriki mara utakapofanyika.
“Haki madini imekuwa msaada mkubwa kwa wachimbaji madini wadogo kwani tumekuwa pamoja bega kwa bega kwa kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata haki zao,” alisema Madiwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger