Meneja
Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, William
Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho,
Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya
tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako
Tanga. Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya
maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani
Afrika na Asia.
Waziri wa
Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko
kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati
alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana
Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.
Waziri
wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja
Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William
Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa
yanayofanyika Tanga.
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna
mkonge unavyoweza kutengeneza dawa pamoja na mafuta aina mbalimbali.
Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga.
Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
SHARE
No comments:
Post a Comment