Mmmoja wa wahitimu wa mafunzo ya mpango wa Mwanamke wa wakati Ujao ,Warda
Kimaro kutoka TBL Group,akipokea cheti kutoka kwa Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako
wakati wa mahafali yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam ,kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri nchini,Mh.Almas Maige.
Mmoja wa wahitimu kutoka TBL Group,Neema Arora akipokea cheti baada ya kuhitimu na kufaulu mafunzo ya kozi hiyo
Meneja
wa ukuzaji vipaji wa TBL Group,Lilian Makau Galinoma akitoa mada wakati
wa hafla hiyo ya mahafali ya kozi ya Mwanamke wa Wakati Ujao
Warda na Neema wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea vyeti vyao
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo haya katika picha ya pamoja
Wahitimu
kutoka TBL Group (walioshika vyeti) wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wenzao walioungana nao katika mahafali iliyofanyika katika
hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
……………………………………………………………………………………..
-Kuzidi kutoa fursa sawa za uongozi ndani ya kampuni
Kampuni
ya TBL Group imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuunga mkono jithada za
kuwajengea uwezo wafanyakazi wake wanawake kwa kuwawezesha kushiriki
mafunzo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya mpango wa ‘Mwanamke wa wakati
ujao’ yanayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana
na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises (NHO)
Akiongea
wakati wa mahafali ya pili ya mafunzo hayo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam,mwishoni mwa Wiki ,Meneja wa ukuzaji vipaji wa TBL Group,Lilian
Makau Galinoma ,alisema kampuni itaendelea kuwa mdau wa mafunzo haya kwa kuwa moja ya dhamira yake kupitia mpango wa Women Working Group ni kuwajengea uwezo
wafanyakazi wake wanawake na kuwapatia fursa za uongozi wa vitengo
mbalimbali ambapo wanaendelea kufanya vizuri na kudhihirisha kuwa ujuzi
hauna jinsia.Mgeni rasmi katika mahafali hayo alikuwa ni Waziri wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce Ndalichako.
“Programu hii ni nzuri hususani kwa wanawake kwa kuwa mafunzo wanayoyapata yanawaongeza uwezo wa kujiamini na
yanaendeshwa zaidi kwa vitendo kuliko nadharia na kuna haja ya kuwa na
programu nyingi za aina hii ili ziwafikie wanawake wengi popote walipo
nchini”.Alisema.
Wafanyakazi
wa TBL Group ambao ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo,Warda
Kimaro na Neema Arora walieleza katika mahojiano jayo kuwa licha
ya kwamba wamepitia vyuo vikuu na kupata mafunzo ya kitaaluma lakini
mafunzo haya chini ya mpango wa ‘ Mwanamke wa wakati Ujao’yamewawezsha
kujua mambo mengi zaidi na kuwajengea uwezo wa kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kazi hususani utawala na jinsi ya kushiriki na kutoa mawazo kwenye vikao vya bodi.
“Nashukuru
wajiri wangu TBL Group kwa kunipatia fursa ya kushiriki mafunzo haya
ambayo yanafanyika kwa vitendo kwa kuwa nimeweza kujua mambo mengi na natoa wito kwa wanawake popote walipo
kujiendeleza zaidi kielimu kwa kuwa silaha pekee ya kumkomboa mwanamke
ni elimu”Alisema Warda ambaye ni Meneja wa Chapa katika kiwanda cha TDL.
Kwa
upande wake Neema Arora alisema kuwa anatamani zingekuwepo programu
kama hizi nyingi hapa nchini kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupata
mafunzo ya nadharia na vitendo kwenye fani mbalimbali ili kuwawezesha
kujikwamua kiuchumi ‘Programu hii ni nzuri na imeniwezesha kupata
maarifa zaidi hususani katika masuala ya utawala,naishukuru TBL Group
kwa kuwa na mkakati wa kuwapatia wanawake fursa za uongozi ndani ya
kampuni”.Alisema Neema ambaye ni Mpishi Mkuu wa kiwanda cha Darbrew.
Akitoa
historia ya mafunzo yanayotolewa chini ya mpango huo,Mkurugenzi wa
ATE,Dk.Aggrey Mlimuka alisema yanaendeshwa na taasisi hiyo kwa
kushirikiana na taasisi ya Confederation of Norwegian Enterprises na
hapa nchini yanaendeshwa kwa kushirikiana na chuo cha Eastern and
Southern African Management Institute (ESAMI)
kilichopo mkoani Arusha na zaidi ni ya vitendo kuliko nadharia
“Wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya mpango huu wanaweza kukutana
darasani katika siku 14 ndani ya kipindi cha miezi tisa zaidi ya hapo wanakuwa
wanajisomea na kufanya kazi kwa vitendo katika sehemu zao za kazi na
wanapofikia mwisho wa mafunzo wanafanya mitihani na kutunukiwa vyeti kwa
wale wanaofaulu”.Alisema.
Waziri
wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,Profesa Joyce
Ndalichako, alipongeza wadau wote wanaofanikisha mafunzo haya na alitoa
wito kwa taasisi mbalimbali kuwapatia wanawake nafasi ya kupata mafunzo
haya ili yawawezeshe kuwa na uwezo wa kushika nafasi za uongozi wa juu
katika sehemu zao za kazi kwa kuwa dunia ya sasa inahitaji elimu ya
kisasa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuleta ufanisi
katika sehemu za kazi
SHARE
No comments:
Post a Comment