TRA

TRA

Thursday, May 25, 2017

ZANTEL KUTOA OFA KWA WATEJA WAKE KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




·         Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo  mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia vifurushi cha kimataifa cha uarabuni.

Tunapokaribia mwezi mtukufu wa Ramadhani, kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini  wanapoelekea kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.

Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bwn. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana  na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.

Bwn. Janin ameelezea kwamba kutakua na bidhaa mbalimbali zitakazotolewa katika kipindi hiki na anawasihi wateja wa Zantel wavipe kipaumbele bidhaa hizi. Ofa hizi zitaanza rasmi tarehe 26/5/2017.

Akielezea Zaidi kuhusu ofa hii, Meneja wa bidhaa na mawasiliano Bi. Rukia Mtingwa amesema “Ofa hii itashirikisha vifurushi vya Bonga na Mpakabasi ambapo wateja wa Zantel watapata punguzo la asilimia 50 kupiga simu kuanzia saa 5usiku hadi saa 11 asubuhi na Zaidi wataweza kupata huduma zetu mpya tulizozindua hivi karibuni kama ‘ZanteL Madrassa’ ambapo wateja wanaweza kupata mufunzo ya dini ya kiislamu kama Quran, Hadith, duah, habari za bakwata, na huduma nyingine nyingi zinazopatikana kupitia kupiga simu, ujumbe wa maneno na programu za simu”.

Bi.Mtingwa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi  kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu  Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 10 kupiga simu kwenda kwenye  nchi tajwa, na fedha hizi zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti za salio za wateja.

Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya ‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586

Zantel inaendelea na mradi wake wa kuboresha mtandao wake kuwa wa kisasa Zaidi visiwani Zanzibar ili kuhakikisha wateja wake wanafurahia huduma zinazoaminika Zaidi zikiwemo huduma ya mtandao wa intaneti wa kasi Zaidi wa 4G, na kwa mara ya kwanza huduma za kibenki za KIISLAM kupitia simu za mkononi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger