Kiungo wa
zamani wa Newcastle, Cheick Tiote ameanguka ghafla na kupoteza maisha
akiwa mazoezini.Tiote amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 30,
alikuwa mazoezini katika kikosi cha Beijing Enterprises kinachoshiriki
ligi daraja la pili.Kiungo huyo raia wa Ivory Coast amejiunga na timu
hiyo miezi mine tu iliyopita.Alikimbizwa hospital zikiwa ni juhudi za
kuokoa maisha yake lakini haikuwezekana.Tiote amewahi kuwa kiungo
tegemeo wa timu ya taifa ya Ivory Coast iliyokuwa inaongozwa na Didier
Drogba.
SHARE
No comments:
Post a Comment