Tayari
mvutano kati ya Manchester United na Real Madrid kuhusu David De Gea
umeanza upya,Madrid wanamtaka De Gea kwa nguvu zote lakini United hawako
tayari kumruhusu De Gea aondoke United.Inasemekana wiki iliyopita klabu
ya Manchester United iliitolea nje ofa ya Real Madrid ya thamani ya
zaidi ya £50m na kuwataka Madrid waende wakajipange zaidi.
Sasa
Jose Mourinho ameona isiwe kesi kwa kuwa wana kipa mwingine mzuri
Sergio Romero baasi ameamua kuwapa Real Madrid ofa ili wampate David De
Gea huku akiwapa masharti.
Mourinho
amewaambia Real Madrid hata wasilete pesa kubwa ila kiasi cha £22m
kinatosha kabisa kwa wao United kumruhusu De Gea ajiunge Real Madrid.
Lakini
kama ulidhani Mourinho anataka £22m tu baasi utakuwa umekosea sana
kwani Mourinho anahitaji kiasi hicho cha pesa pamoja na mchezaji Alvaro
Morata.
Kama
Real Madrid watatoa kiasi hicho cha £22m pamoja na Morata ambaye hapewi
sana namba katika kikosi cha Madrid baasi United watakuwa tayari
kumuacha De Gea aondoke.
Kama
Madrid watakataa kumtoa Morata baasi itabidi watoe kiasi kikubwa cha
pesa kwani United inasemekana wanataka kiasi cha £66m kumnunua De Gea.
SHARE
No comments:
Post a Comment