…Akiongea jambo na lafiki yake huku akiwa na familia yake. MIEZI
kadhaa iliyopita, Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliwahi
kunukuliwa akisema kuwa kwa jinsi serikali yake inavyofanya kazi,
ikiwemo kutoa elimu bure, akawapa ruhusa wanandoa kuendelea kutafuta
watoto ambapo alitumia neno kufyatua.Neno
hilo limekuwa maarufu kutokana na alivyolitumia kiongozi huyo, hivyo
kwa mwenendo wa sasa unavyoelekea kwa mshambuliaji staa wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo ni kama ameamua kufyatua tu katika suala la kutafuta
watoto.
Mshambuliaji staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akiwa na familia yake.
Akiwa na
umri wa miaka 32, kwa sasa ni baba wa watoto watatu, wawili akiwa
amewapata mwaka huu na anatarajiwa kumpata wa nne baadaye mwaka huu.
Akiwa kamshika mpenzi wake.
Inakumbukwa
kuwa, mtoto wake wa kwanza anayejulikana kwa jina la Cristiano Jr
mwenye umri wa miaka saba, alizaliwa Juni 2010 huku mama yake akiwa
hajulikani kwa mashabiki wa mchezaji huyo.
Ndivyo
ilivyokuwa kwa pacha wake wa mwaka huu ambao ni Eva na Mateo, nao
wamezaliwa nchini Marekani kama ilivyokuwa kwa kaka yao huku Ronaldo
akiwa mgumu kutaja mama wa watoto hao.
Kuelekea
kumpata mtoto wake wa nne, ameamua kubadili staili kutoka ya usiri wa
mama mtu na sasa mtoto huyo anatarajiwa kupatikana kupitia kwa mchumba
wake, Georgina Rodriguez ambaye ana ujauzito.Ronaldo alithibitisha juu
ya ujauzito huo juzi baada ya kuwepo kwa tetesi nyingi kuwa mrembo huyo
ni mama kijacho. Staa huyo wa Madrid ambaye ni raia wa Ureno,
alithibitisha kwa kukiri kuwa ni kweli na anafuraha kumsubiri mwanaye
huyo.
Georgina,
23, amekuwa akionekana maeneo tofauti huku ‘kitumbo’ kikiwa kimetuna
ambapo mama yake Ronaldo aliwahi kukana kuwa mkwewe huyo siyo mjamzito.
WalipoanziaKabla
ya kukutana na Ronaldo, Georgina alikuwa ni mfanyakazi wa maduka ya
Gucci kwenye Jiji la Madrid.Akiwa katika pitapita zake za masuala ya
mitido, ndipo Ronaldo alipokutana na mrembo huyo kwenye tamasha moja la
maonyesho ya mavazi.
Wakiwa
huko, ndipo walipobadilishana namba na kuanza kuwasiliana, uhusiano wao
ulianza kwa siri kabla ya baadaye kunaswa wakiwa pamoja nchini Ufaransa.
Haijajulikana
uhusiano wao ulianza lini hasa lakini mara ya kwanza wanaonekana
hadharani pamoja ilikuwa Novemba, 2016.Anakubalika na familiaLicha ya
kujulikana wazi kuwa Ronaldo ametokea kwenye familia ya kimasikini,
alipambana na kupata utajiri mkubwa, baada ya miaka mingi ya kufanya
starehe huku akifanya kazi ambapo miradi mingi ilikuwa ikisimamiwa na
mama na dada yake, inavyoonekana sasa anahitaji mke na watoto kwa ajili
ya kuendeleza familia na utajiri wake.
Awali
ilionekana bado hajapata mwanamke sahihi na ndiyo maana hata aina ya
utafutaji wa mtoto wake wa kwanza na hawa wawili aliowapata mwaka huu
aliufanya kwa kificho huku mama zao wakiwa hawajulikani.Kitendo cha
kumtambulisha Georgina kinamaanisha kuwa amemkubali na kuna tetesi kuwa
wawili hao wanaweza kufikiria juu ya kufunga ndoa baada ya kujifungua.
Akiongozana na mpenzi wake.
Kuonyesha
anamkubali, wiki kadhaa zilizopita Ronaldo alipiga picha akiwa na
familia yake pamoja na ndugu zake wengi wakiwa pamoja wanaogelea kwenye
bwawa la nyumbani kwa mchezaji huyo.
Licha ya
kuwa mama wa watoto watatu wa sasa wa Ronaldo hawajulikani, lakini
Georgina amekuwa akionekana kuwa pamoja na watoto hao kama vile yeye
ndiye mama watoto.
Kuhusu
mama wa watoto wake, Ronaldo aliwahi kunukuliwa akisema: “Kwa
makubaliano niliyonayo, kuhusu mama hilo litabaki kuwa siri kwa watoto
wangu.”
Wakati
timu ya Real Madrid ikiwa imeshaanza mazoezi kujiandaa kwa msimu ujao,
kwa sasa Ronaldo ana muda mwingi wa kuwa na familia yake hiyo kwa kuwa
yupo katika mapumziko baada ya kumalizika kwa msimu wa 2016/17 kisha
akaenda kuitumikia Ureno kwenye michuano ya Kombe la Mabara.
SHARE
No comments:
Post a Comment