Ghetto Kids wakiweka pozi.
Moyo wa
subira, juhudi na ubunifu ndiyo kila kitu katika maisha ya mtu mwenye
shauku ya mafanikio. Hicho ndicho kilichowafikisha watoto wa Ghetto Kids
kwenye kilele cha mafanikio barani Afrika na duniani.
Kwa sasa watoto
hawa wameula, wanaogelea kwenye fedha. Dunia inawajua na wana mvuto wa
kipekee wanapokabidhiwa jukwaa kufanya mambo.
Ghetto Kids, hatari.
KAMA UTANI VILE
Ghetto
Kids walianza kuonekana kama utani vile kwenye mitandao ya kijamii
wakicheza muziki kwa staili ya aina yake kwa kutumia Wimbo wa Maria Rosa
wa mwanamuziki, Eddy Kenzo wa Uganda, tena kwa staili ya kuchekesha na
kivituko zaidi.
Walikuwa
wakicheza muziki wa video kali zilizotoka na zilizoonekana kuwashika
mashabiki wengi duniani, hasa kwa kuzingatia jina la mwanamuziki husika
aliyeachia ngoma yake.
Ghetto Kids wakiwa na French Montana.
COVERS ZA NGOMA KALI
Mbali na
kufanya covers (kurudia video za nyimbo kwa staili tofauti) za video za
Kenzo pia walifanya za ngoma kali za mastaa wakubwa duniani kama Sorry
ya Justin Bieber, Make Am ya Patoranking na nyingine kibao huku
wakitamaniwa na mastaa wengi kama Nicki Minaj na French Montana
aliyediriki kusema kuwa wanajua kucheza zaidi ya Chris Brown.
Nikiri
kuwa, nilipoona video zao kwa mara ya kwanza kwenye mitandao ya kijamii,
nilivutiwa na staili yao hiyo ya kucheza muziki mitaani kwa mpangilio
wa aina yake, wakionekana wachafu kwa kujigaragaza kwenye mavumbi na
matope.
Ghetto Kids.
MAISHA HALISI
Kilichonivutiwa
zaidi kwa watoto hawa ni namna walivyoakisi mazingira ya Kiafrika na
maisha halisi ya sehemu kubwa ya bara hilo. Mavazi yao yanayowaonesha
kama vile wanatoka familia zisizokuwa na uwezo kiasi cha kuvaa mavazi
yaliyochanika na kuwekewa viraka kuonesha maisha ya familia nyingi
ambazo hazina uwezo wa kuwanunulia watoto wao nguo mpya.
Ghetto Kids wakiwa katika picha ya pamoja.
GETTO KIDS NI AKINA NANI?
Kadiri
siku zilivyosonga ndivyo walivyozidi kuwa gumzo mitandaoni. Hapo ndipo
nilipopata shauku ya kutaka kujua Getto Kids ni akina nani?
Jina
kamili la kundi lao ni Triplets Ghetto Kids kutoka nchini Uganda. Kundi
hilo linaundwa na watoto ambao wote wamezaliwa baada ya mwaka 2000 (yupo
aliyezaliwa 2010). Baadhi yao ni pamoja na Ada, Patricia, Ashley, Man
King, Ronnie, Isaac, Fredy, Nyangoma, Kokode na wengineo. Mwaka 2014
walipata pigo la kufiwa na mwenzao kwenye ajali ya baiskeli aliyeitwa
Alex.
Patricia.
WANAMILIKIWA NA EDDY KENZO
Kwa mujibu wa mwanamuziki wa Uganda anayelimiliki kundi hilo, Eddy Kenzo, watoto hao aliwakusanya mitaani wakiwa hawajuani.
Wengi wao
ni watoto waliokulia maisha magumu ya mitaani kutokana na familia zao
kutokuwa na uwezo wa kuwapeleka shuleni au kuwapa malezi bora. Pia
baadhi yao ni yatima.
Kenzo
anasema kuwa, tangu kuanza kwa safari yao ya ku-dance mavumbini na
kwenye matope, walionekana watoto wa mitaani wasiokuwa na mwelekeo wa
kimaisha.
Eddy Kenzo.
KENZO AONA TOBO
Ilibidi
kutumia staili hiyo baada ya kubaini kuwa, kuna tobo au mwanya ambao
wengi hawauoni. Kwamba, staili hiyo inaakisi uhalisia wa familia zilizo
nyingi za Kiafrika na kwamba ingepata mvuto kwa sababu ni staili ya
kipekee.
Kenzo ni
mwanamuziki mkubwa nchini Uganda hivyo anasema si kweli kwamba
alishindwa kuwapiga sopusopu na pamba kali za kisanii, lakini alitaka
waonekane hivyo kuleta utofauti na ndiyo maana wakiwa nje ya steji au
kazi yao hiyo wanaonekana ni watoto wa matajiri f’lan.
WAPENYA ULAYA, MAREKANI
Mdogomdogo,
Ghetto Kids walianza kuiteka Uganda, Afrika Mashariki na Afrika kwa
jumla. Baadaye walivuka mipaka ya Bara la Afrika. Wakaanza kulamba shoo
mabara mengine, wakialikwa kwenye matamasha makubwa ya Ulaya na Amerika
(Marekani).
Sasa
maisha ni bomba. Wanatamba hadi Hollywood, Marekani. Mwaka huu
walipafomu kwenye moja ya steji kubwa za kimataifa na kutumbuiza mbele
ya umati mzito wenye macho ya wasanii wakubwa na watu mashuhuri duniani
kwenye tuzo kubwa za BET za Marekani.
French Montana.
FRENCH MONTANA AWAONA
Katika
harakati zao hizo, walionekana na staa mkubwa wa muziki wa Marekani,
French Montana. Staa huyo alipowaona watoto hao, aliamua kuwatumia
katika tour (ziara za kimuziki) sehemu mbalimbali duniani.Mbali na hilo,
pia wamekuwa wakipata coverage (kuandikwa) kwenye majarida makubwa ya
burudani kama Vibe la Marekani.French Montana amewatumia pia kwenye
video ya ngoma yake kali ya Unforgettable aliyomshirikisha Rapa Swae Lee
ambayo imetazamwa na zaidi ya watu milioni 170 kwenye Mtandao wa
YouTube.
DOLA LAKI 1 KUWASAFIRISHA
Kupitia
Jarida la Vibe, French Montana anasema kuwa, baada ya kuwaona watoto hao
kwenye mitandao ya kijamii, alitumia kiasi cha dola laki moja (zaidi ya
Sh. milioni 220) kuwasafirisha kutoka Uganda hadi Marekani kwa ajili ya
kuwatumia kwenye kazi zake za kisanaa.
“Stori
yao ni ya aina yake, jinsi walivyokutanishwa na namna wanavyoishi
pamoja,” anasema French mwenye asili ya Morocco na kuongeza;.
“Unforgettable
(ngoma yake) haikuwa ngoma yangu pekee. Nilipenda kuwaona watoto hawa
wakiwa na furaha. Ukweli ninapenda kuwaona sasa wana furaha.”
SHARE
No comments:
Post a Comment