MJASIRIAMALI
mdogo mkazi wa Chanika, jijini Dar es Salaam,
Enos Marianus, amesema bahati nasibu ya Biko inayaoendelea kuchanja
mbuga
nchini Tanzania, utakuza uchumi wa washiriki na Watanzania kwa ujumla,
akiwamo yeye ambapo ana mpango wa kuendeleza biashara zake..
Hayo yamesemwa na mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Marianus
wakaati anakabidhiwa fedha zake katika makabidhiano yaaliyofanyika jana katika
benki ya NMB, Posta, jijini Dar es Salaam.
Marianus alisema ukosefu wa ajira unasababisha watu wengi
watamani kuingia kwenye ujasiriamali, hivyo uwapo wa mchezo wa Biko utapunguza
changamoto hiyo, hivyo ni jambo la msingi la kuhakikisha kuwa kila mtu anacheza
Biko ili ashinde mamilioni ya Biko.
“Nashukuru leo kwa kukabidhiwa fedha zangu Sh Milioni 20
kutoka kwa watu wa Biko, hivyo ninaamini kabisa mchezo huu utakuza uchumi wetu
hususan sisi wajasiriamali wadogo ambao fedha hizi zitaingia kwenye kupanua
wigo wa biashara zetu kwa namna moja ama nyingine,” Alisema.
Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan
Melles, alisema ushindi wa Biko ni rahisi husuan kwa wale wanaocheza mara
nyingi kwa kufanyaa miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel kuanzia
Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba yao ya kampuni ni 505050 na ile ya
kumbukumbu ni 2456.
“Sh 1,000 ya Biko inayochezwa inampa mtu ushindi wa papo kwa
hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni
Moja inayolipwa papo hapo kwenye simu iliyotumika kuchezea Biko pamoja na
zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles.
Zaidi ya Sh Bilioni moja tayari zimelipwa kwa washindi wa
Biko kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, ikiwa ni mwendelezo wa kutoa
mamilioni ya fedha kwa washindi wake wanaocheza Biko tangu kuanzishwa kwa
mchezo huo hapa nchini.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heave wa
pili kutoka kulia akimkabidhi fedha zake mshindi wa Sh Milioni 20 wa
Biko, Enos Marianus mwenye shati jeupe, jana jijini Dar es Salaam,
katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles.
Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles wa
pili kutoka kulia akimkabidhi fedha zake mshindi wa Sh Milioni 20 wa
Biko, Enos Marianus mwenye shati jeupe, jana jijini Dar es Salaam,
katika benki ya NMB. Wa kwanza kulia ni Goodhope Heaven, Meneja Masoko
wa Biko Tanzania.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 24, Enos Marianus kulia aakiwa
na furaha tele baada ya kukabidhiwa fedha zake jana katika benki ya NMB,
jijini Dar es Salaam, siku moja baada yaa kutangazwa mshindi wa bahati
nasibu ya Biko. Kushoto kwake ni mkewe Bi Kisa Kasito aliyemsindikiza
katika kukabidhiwa fedha zake.
SHARE
No comments:
Post a Comment