Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono Mama mmoja mlemavu 
mkazi wa Buseresere mara baada ya kumaliza kuhutubia mamia ya wakazi wa 
Katoro na Buseresere waliojitokeza pembezoni mwa barabara katika eneo 
hilo kumsalimia wakati akielekea Chato Mkoani Geita jana jioni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Bwanga njia 
panda ya kuelekea Makao makuu ya Wilaya ya Chato jana jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katoro na 
Buseresere mara baada ya kusimama wakati akielekea Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Geita mjini wakati akielekea Chato.
Wananchi wa Geita waliokuwa na 
Shauku ya kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John 
Pombe Magufuli wakiwa wamepanda juu ya magari pembezoni mwa barabara ya 
Usagara-Sengerema-Geita jana jioni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mama Rosemary Lucas 
ambaye alikuwa akiwasilisha kero yake ya kuvunjiwa nyumba Sengerema 
mkoani Mwanza.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John 
Mongela akichukua maelezo ya mama huyo Rosemary Lucas aliyevunjiwa 
nyumba yake Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa zamani wa 
CHADEMA Hamis Tabasamu ambaye alikuwa akionesha Kadi yake mpya ya CCM 
mara baada ya kuhamia. Kadi hiyo alikabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa 
wa Mwanza katika Wilaya ya Sengerema. 
(PICHA NA IKULU)
  SHARE 
  
 
 








 
No comments:
Post a Comment