 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Nuru Luvinga
 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Nuru Luvinga
BWANA Sukulu Mageta akiwa na mkewe Diana
 wote wajasiriamali wakiwa na watoto wao, Msuya S Mageta (18) na 
Ng'washi S Mageta, aliamua kutumia muda wake mchache kutembelea banda la
 Mfuko wa Pensheni wa PPF, ili kujua nini hasa anachoweza kufaidika 
nacho endapo atajiunga na Mfuko huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, 
Bi. Jannet Ezekiel ndiye aliyekuwa na jukumu la kutoa "darasa" kuhusu 
faida za kujiunga na PPF kupitia mpango wa WOTE SCHEME, ambao ni maalum 
kwa wanachama wanaojiunga kwa uchangiaji wa hiari, mpango unaowahusu 
wajasiriamali, mama lishe, bodaboda na mgtu yeyote anayefanya kazi ya 
kumuingizia kipato na uwezo wa kuchangia kila mwezi angalau shilingi 
elfu 20.
Bi Jannet aliieleza familia hiyo kuwa mwanachama wa mpango wa wote scheme,
 atafaidi Mafao mbalimbali yakiwemo, Mafao ya afya,  Mkopo wa Elimu, na 
Mafao mengine mengi. Baada ya kupatiwa elimu hiyo, Bw. Sukulu aliamua 
kumuandikisha kijana wake wa mika 18 Msuya S. Mageta kujiunga na mpango 
huo wa WOTE SCHEME, kwa lengo la kujiwekea akiba ili afaidike na Mkopo 
wa elimu.
 Bi Jannet Ezekiel, (kushoto), 
akimkabidhi fomu ya kujiunga na Mpango wa WOTE SCHEME, kijana Msuya S. 
Mageta. Katikati ni baba mzazi wa Msuya, Bw. Sukulu Mageta 
Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PPF, Bi. Pauline Msanga, akichapa kazi
 Afisa Msaidizi Huduma kwa Wateja, Bw. Mohammed Siaga, akichapa mzigo
 Afisa Mtafiti wa PPF, Bi.Elaine Maro, 
(kulia), akimpokea kwa bashasha mwanachama huyu aliyefika kupatiwa 
taarifa zamichango yake
 Baada ya muda mchache mwanachama huyo anapata taarifa yake na ufafanuzi pia
 Afisa Mafao wa PPF, Bi. Tulla Mwigune, (kushoto), akimpatia maelezo mwanachama huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huu
 Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akimkabidhi kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia WOTE SCHEME, Bw.Martin Mtenga.
  SHARE 
  
 
 
















 
No comments:
Post a Comment