Darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 lililojengwa na kampuni ya Tigo kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa, |
Wazazi wakishudia makabidhiano ya darasa lenye thamani ya Milion 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi wilayani Kondoa. |
…………………………………………………..
Kondoa Dodoma – Kampuni
ya maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania Tigo, leo imekabidhi
darasa lenye thamani ya shilingi milioni 8.5 kwa shule ya msingi Hachwi
iliyoko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma katika juhudi za kusaidia ukuaji
wa kiwango cha elimu wilayani humo.
Akiongea
katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika shuleni hapo, Mkurugenzi wa
Tigo wa Kanda ya Kaskazini George Lugata alisema kwamba mchango huo
ulikuwa ni sehemu ya juhudi za wafanyakazi wa Kampuni kujitolea na
jukumu la kampuni kusaidia maendeleo ya jamii (CSR) katika kusaidia
elimu Tanzania.
“Tigo
ina sera nzuri ya (CSR) ambayo inasisitiza katika kutoa kwa ajili ya
kusaidia Jamii ambako kampuni inaendesha shughuli zake. Tunaamini kwamba
kupitia mchango huu, Tigo itakuwa imechangia kwa mara nyingine katika
kutengeneza mazingira kwa ajili ya ukuaji wa wataalamu wa baadae kwa
ajili ya maendeleo ya haraka ya nchi”, alisema Lugata.
Katika
nafasi yake Meneja wa CSR wa Tigo, Bi Halima Okash, aligusia
vipaumbele vya kampuni vya uwekezaji katika jamii, akisema kwamba Tigo
ilikuwa tayari kushirikiana na wadau wengine wenye fikra kama hizo
katika juhudi zake za kusaidia maendeleo ya jamii.
Kupitia
mpango wetu wa uwekezaji katika jamii, Tigo imekuwa katika mstari wa
mbele kuinua sekta ya elimu nchini ambapo tumeshatoa komputa na
kuunganisha shule 60 za sekondari kwenye mtandao wa intaneti wenye kasi
zaidi kupitia mradi wetu wa e-school pamoja na kuchangia zaidi ya
madawati 7,000 kwa shule za msingi nchini kote”alisema Okash.
Mgeni
rasmi katika sherehe, Mkuu wa mkoa wa wilaya ya Kondoa, Sezeria Makutta
aliishukuru Tigo kwa mchango wake, akibainisha kwamba itasaidia sana
katika kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja, ambapo
itatengeneza mazingira mazuri ya kujifunzia shuleni.
“Tunawashukuru sana Tigo kwa msaada wao”, alisema Makutta, akiongeza kwamba; “Tunawaomba watu wengine wenye moyo wa kujitolea kujitokeza na kuongeza nguvu katika kuondoa upungufu wa madarasa katika wilaya yetu”.
SHARE
No comments:
Post a Comment