Mfuko moja uliotumika na mwananga Neil Amstrong kukusanya violezi vya mwezi umeuzwa kwa dola milioni 1.8 mjini New York.
Mfuko huo kutoka kwa chombo cha angani Apolo 11 mwaka 1969 ulinunuliwa katika eneo la Sotheyby na mtu asiyejulikana.
Mfuko huo bado una vumbi na mawe madogo madogo kutoka mwezini.
Mnada huo
unajiri baada ya mapambano mahakamani kuhusu umiliki wa kifaa hicho cha
kipekee kutoka kwa ujumbe wa Apollo 11 ambao ulikuwa katika mikono ya
mtu binafsi.
Baada ya chombo hicho cha angani kurudi duniani, vifaa vyote vilipelekwa katika jumba la makumbusho la Smithsonian.
Hatahivyo mfuko huo uliachwa katika boksi katika kituo cha vyombo vya angani cha Johnson kutokana na makosa ya kihesabu.
Baadaye haukutambulika wakati wa mnada wa serikali, ukiuzwa kwa dola 995 pekee kwa wakili mmoja wa Illinois 2015.
Hatahivyo
mamlaka inayosimamia vyombo vya angani Nasa ilijarabu kuuchukua mfuko
huo, lakini mapema mwaka huu jaji mmoja aliamuru kwamba ulimilikiwa na
mnunuzi huyo kimakosa ambaye baadaye ailiupeleka katika mnada huo wa
Sutheby
SHARE
No comments:
Post a Comment