Mshambuliaji Alvaro Morata amefanikiwa kusaini mkataba rasmi wa kujiunga na Chelsea.
Morata
ambaye ametokea Real Madrid ya Hispania amesaini mkataba wa kujiunga na
mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza kwa msimu uliopita kwa mkataba wa
miaka mitano.
Hata
hivyo dau la uhamisho wa mshambuliaji huyo limekuwa na utata ndani yake
huku gazeti la Telegraph likidai mchezaji huyo amesajiliwa kwa paundi
milioni 80 huku vyombo vingine vikidai amesajiliwa kwa paundi milioni
70.
SHARE
No comments:
Post a Comment