Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (aliyesimama),
akiongea na watumishi, kutoka katika vituo 19 vya vivuko nchini vinavyosimamiwa
na TEMESA. Watumishi hao walikua wakiagana na Dkt. Mgwatu baada ya kumaliza mafunzo
yao yaliyotoleawa na Chuo cha Bahari cha jijini Dar es Salaam (DMI).
NA THERESIA MWAMI
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, akizungumza na watumishi
mbalimbali kutoka kwenye vituo vya vivuko nchini vinavyosimamiwa na TEMESA waliohudhuria
mafunzo katika Chuo Cha Ubaharia cha Dar es Salaam.
Dkt. Mgwatu amewataka watumishi
hao wa kada ya ubaharia pamoja na unahodha wa vivuko kwenda kuyatumia mafunzo
hayo kwa vitendo na kuwa waadilifu na pia kutoa kauli nzuri kwa wateja
wanaotumia huduma za TEMESA. Aidha Dkt. Mgwatu ameahidi kufuatilia kwa haraka
suala la kuboresha mikataba ya ajira kwa watumishi wa muda ili wapate mikataba
ya mwaka mmoja badala ya miezi mitatu kama ilivyo hivi sasa.
Awali katika taarifa yake
Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko TEMESA, Mhandisi
Japhet Maselle, alisema kuwa watumishi 46 wamepatiwa mafunzo katika Chuo cha Ubaharia
kwa muda wa wiki mbili na kuwa miongoni mwa kozi walizozisoma ni pamoja na “Refresher
Course”, “Mandatory Course”, “Rating Course”pamoja na “Ship Security Course. Lengo
hasa la mafunzo hayo ni kuboresha huduma za vivuko zinazosimamiwa na TEMESA
nchini.
TEMESA ina jumla ya vivuko
29 katika vituo 19 pamoja na boti 4 ndogo zinazotumika nyakati za dharura.
Baadhi ya
Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) waliomaliza mafuzo katika Chuo
cha Bahari (DMI) wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa TEMESA (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam.(Picha na Theresia
Mwami)
Mkurugenzi
wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle (aliyesimama kushoto) akisoma taarifa ya
mafunzo yaliyotolewa kwa baadhi ya Mabaharia na “Ferry Captains” 46 wa TEMESA
kutoka katika vituo 19 vya Vivuko vinavyosimamiwa na wakala huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment