Barcelona
wanakaribia kumfanya mchezaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele
mchezaji wa pili aliye ghali zaidi katika historia.
Kitita hicho hatahivyo kinakadiriwa kuwa chini ya Yuro milioni 222 ambazo PSG iliilipa Barcelona kumnunua Neymar mnamo mwezi Agosti.
Ousmane Dembele wa Borrusia Dortmund
Hathivyo kitita hicho kitakipiku kile kilichotolewa na Manchester United kumnunua Paul Pogba kutoka Juventus.
Mchezaji wa Ufaransa Dembele hajaichezea Dortmund tangu kombe la Supercup mnamo tarehe 5 Agosti.
Alijiunga na timu hiyo ya Bundesliga kutoka klabu ya Rennes kwa Yuro milioni 15 miezi 12 iliopita akiwa ameanza kucheza mwaka 2015.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment