Kocha wa Yanga, George Lwandamina hana mpango wa kuondoka, maana tayari ameongezewa muda wa kuendelea kufanya kazi Jangwani.
Uongozi wa Yanga umeamua kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja
kocha wake George Lwandamina raia wa Zambia baada ya ule wa awali
kumalizika Julai 16, mwaka huu.
Katika mkataba wake
uliopita, Lwandamina aliiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara
msimu uliopita na kuifikisha katika nusu fainali ya Kombe la FA kabla ya
kutolewa na Mbao FC ya Mwanza.
Katibu Mkuu wa Yanga,
Boniface Mkwasa amesema mchana kuwa, wameamua kumuongezea mkataba
Lwandamina baada ya kuridhishwa na kazi yake.
“Tunaingia mkataba
mwingine wa mwaka mmoja na Lwandamina kwani ule wa mwanzo umeisha na
sasa kila kitu kipo tayari hivyo muda wowote tena kwa uwazi kabisa
atasaini mkataba mpya.
“Tumejitahidi kwa
uwezo wetu kuboresha mkataba wake mpya kwa kumuongezea maslahi kidogo
ili apate motisha ya kufanya kazi yake ipasavyo,” alisema Mkwasa.
Lwandamina
alitarajiwa kusaini mkataba huo muda wowote kuanzia jana mchana ili awe
na uhakika wa kuendelea kufanya kazi yake kwa uhuru na kujiamini.
SHARE








No comments:
Post a Comment