TRA

TRA

Saturday, August 26, 2017

Makamu wa Rais Ahudhuria Kilele cha Miaka 50 ya NBC

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Bodi na Menejimenti ya NBC na Mabenki mengine kuwa kuanzia sasa Taasisi zote za fedha ziweke kipaumbele cha kwanza katika kuwezesha kuendeleza viwanda nchini hasa viwanda vidogo vidogo na vya kati vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, misitu na madini ambayo yanapatikana kwa wingi hapa nchini.Pia viwanda ambavyo vinatumia teknolojia ya kati na nguvu kazi zaidi ( labour intensive technology).
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubua kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya NBC.
Mhe. Samia alisema mabenki mengi yameendelea kutoza riba ubwa hivyo kupelekea wananchi wa kipato cha chini hivyo aliwataka Wataalamu wa NBC na Sekta za Fedha kwa ujumla kutafuta suluhisho la riba zisizo rafiki kwa walio wengi ili amana pamoja na mikopo iweze kuongezeka.
Makamu wa Rais aliziagiza Bodi na Menejimeni ya NBC na Mabenki yote nchini kuzingatia Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, alisema ” Serikali ya Tanzania haitomuonea mtu haya na itachukua hatua kali dhidi ya benki au Taasisi yeyote itakayobainika kukiuka matakwa ya sheria hiyo.”
Mwisho Makamu wa Rais aliipongeza benki ya NBC kwa kuweza kutoa gawio la Shilingi Bikioni 1.2 mwaka huu 2017 kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger