Na Mahmoud Ahmad Monduli
Wilaya
ya monduli bado inakabiliwa na changamoto kubwa la ongezeko la mimba za
utotoni ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wanafuzni 45 shule za msingi
walipata ujauzito na 33 wa shule za sekondari kuanzia mwaka 2015 hadi
july 2017 ambapo wanafunzi hao wameacha shule kutokana na hali hiyo
ambapo imewarudhisha nyumba katika kupambana na adui ujinga.
Hayo
yameelezwa leo na Afisa elimu sekondari Rebeca Mbaga wakati
akiwasilisha taarifa fupi katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na
mimba za utotoni iliyofanyika katika wilaya ya monduli ambapo ilihusisha
wadau mbalimbali wa elimu ikiwemo wanafunzi wa shule zamsingi na
sekondari kutoka wilayani hapo ,mkoa wa arusha.
Hata
hivyo alisema kuwa lengo hasa la kuzindua kampeni hiyo nikutaka
kuangalia namna ya kuzuia tatizo hilo lisiendelee na kuchukua hatua kali
kwa wale wotye wanajihusisha na mapenzi na watoto washule na
kuwadanganya na kuwakatiza ndoto na masomo yao.
Aidha
aliongeza kuwa takwimu hizo nikubwa ukilinganisha nakipindi kifupi cha
watoto hao kukaa mashuleni hata hivyo amewataka wadau kuwa walizni na
kuwasaidia kuwabaini wale waliofanya vitendo hivyo viovi ambavyo
vinaenda kinyume na jitihada za Rais kuweza kutoa elimu bure na
kupambana na wale wote wanaowaghilibu wanafunzi na hata kuwakatisha
masomo yao hatua kali zichukuliwe dhizi yao ili iwe fundisho kwa jamii
na familia za watoto.
Kwa
upande wake Mratibu wa huduma za afya na uzazi kutoka hospitali ya
wilaya ya monduli Rachel kivumba alisema kuwa takwimu zinaonyesha kuwa
mwaka 2016 kati 8537 kati yao 1936 ambao wako chini ya miaka 20 walipata
ujauzito na mwaka 2017 kati ya 3875 kati yao 851 ambao wako chuini ya
miaka 20 walipata ujauzito na kujifungua mbapo limekuwa tatizo kubwa
ambalo linapotyeza nguvu kazi ya taifa na ndoto za watoto hawa.
Ambapo
madhara yatokanayo na kubeba ujauzito mapema ni kutokomaa kilakili kwa
watoto hawa na nyonga zao na mifupa haijakomaa kuweza kuhimili uzito wa
mtoto kukua akiwa tumboni hali ambayo wengine wanalazimika kufanyiwa
upasuaji na baadhi yao kutokwa na damu nyimgi hata kupelekea kupoteza
maisha yao.
Kwa
upande wake Afisa ustawi wajamii Monduli Denis Mgie alisema kuwa
miongozo na kanuni na sheria za mtoto zinakinzana kama sheria no 21 ya
mtoto ya mwaka 2009 katika kupata haki yake ya kimsingi kwani
inatofautina katika tafsiri ya mtoto kuna haja ya kuweza kurekebisha
upya ili kumwezesha mtoto kupata haki yake.
Kwa
upande wake Mkuu wa dawati la jinsia na watoto kutoka jeshi la polisi
Monduli Regina Wilbert alisema kuwa wanapokea kesi nyingi sana ambapo
mwaka 2016 zlilipotiwa kesi 45 ambapo kati ya hizo kesi 28 zilihusisha
wanafunzi wa shule za msingi ambapo mwaka 2016 kesi 7 tu zilienda
mahakamani na mwaka 2017 kesi zilizoripotiwa nikesi 29 na kati ya hizo
kesi 12 tu zilihusisha wanafunzi wa msingi na kesi 9 zilihusisha
wanafunzi wa sekondari kati ya hizo kesi 4 tu zilienda mahakamani.
Ambapo
ukilinganisha kesi wanazopokea na kupelekwa mahakamani bado kunakuwepo
na changamoto nyingi katika jamii kuweza kukamilisha vielezo vya
kuwapeleka watuhumiwa mahakamani ikiwemo mila potofu ambapo zinakuwa
nichangamoto katika kutoa ushahidi ,kuogopa laana kuotka kwa wazazi
kutowataja waliohusika kuwapa mimba ,uelewa mdogo wa kutunza vielelezo
vya udhalilishaji pamoja mna mhanga kudhalilishwa.
Kwa
upande wake Mbunge wa Monduli Julius Kalanga kupitia chama cha
demokrasia (CHADEMA)alisema kuwa Serikali izingatie dhana ya
ushirikishwaji bila ya kujali tofauti zilizoko katika kutafuta ufumbuzi
wasuala hili la mimba za utotoni kuweza kumaliza tatizo hili amballo
linaonekana kuonekana linaongeza katika wilaya hiyo.
Aliwataka
wazazi kuwa makini katika kuwalinda watoto wao na kushirikiana na
walimu kuweza kuhakikisha watoto wanapata elimu yao ya msingi hadi chuo
kwa wakati na bila ya kuwa na vikwazo vyovyote vinavyoweza kuwakwamisha
kufikia ndoto zao.
Kwa
upande wake mwenyekiti wahalmshauri ya wilaya ya monduli Issack Joseph
kupitia chama cha chadema alisema kuwa alisema kuwa wanasimamia kauli ya
Rais wa nchi ya kuwa mwanafunzi yeyote atakae pata miba hataruhusiwa
kuendelea na masomo hivyo basi amewataka wanafuzni kuweza kusimamia
masomo yao na waweze kujitambua kwa kusoma tu na sio kuchanganya mambo
mengine ambayo wakati wake bado .
Na
amewataka wanafuzni hao endapo mtu yeyote atawalazimisha kufanya kitu
kinyume na utaratibu washitaki kwa uongzi husika ili kuweza kufanyiwa
kazi ili kuweza kuwasaidia watoto hao kupata haki yao ya msingi ya elimu
kwani ndio nguzo ya maisha ya mtoto yeyote mwenye sifa za kupata elimu.
mwisho..
kutoka kwa jamii ambazo wanakuja kushataki lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
SHARE








No comments:
Post a Comment