Fedha hizo zitatumika kwa miaka mitatu ambapo kwa kunzia
sh. bilioni 1.5 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Kwa mujibu wa Meya Sitta, fedha hizo ni swa na asilimia
10 ya mapato yatokanayo na makusanyo ya ndani kwa mwaka ikiwa ni utekelezaji wa
sera inayozitaka halmshauri na
manispaa zote nchini kutenga mifuko maalumu kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi wanawake
na vijana.
Meya Sitta alisema hayo alipozungumza na wakazi wa Kawe
kwenye viwanja vya Tanganyika Packers kuzungumzia kero za huduma mbalimbali za jamii.
Alitoa wito kwa makundi yenye sifa kuchangamkia fursa ya
fedha hizo na kuzifanyiakazi kadri itakavyoelekezwa ili kujikwamua kiuchumi
wakati wa utekelezaji wa mradi yao.
Alisema halmashauri hiyo imeanza kuboresha miundombinu
ya maji, umeme, vyoo, barabara na vibanda vya kisasa ili kuwa na mazingira bora
ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali wadogo katika maeneo iliyotenga kwa ajili
yao.
Meya Sitta aliwaambia wakazi hao kuwa, halmashauri hiyo
imeanza kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) kwa ajili ya
kujenga stendi ya kisasa ya mabasi ya daladala Kawe na maeneo ya wafanyabiashara
wadogo.
“Wafanyabiashara wote walio katika maeneo yasiyo rasmi
kwa biashara na hatarishi watatambuliwa na kuwezeshwa kupitia mpango maalumu wa
mfuko wa kuwawezesha wanawake na vijana unaosimamiwa na manispaa yetu,” alisema
Meya sitta ambaye pia ni Diwani wa Msasani.
Hivi karibuni Rais John Magufuli aliwaagiza viongozi wa halmashauri,
Manispaa, Miji, Mikoa na Wilaya zote nchini kutenga maeneo rafiki na
yanayofikika kwa wafanyabiashara wadogo.
SHARE
No comments:
Post a Comment