Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 12 Agosti, 2017 amempongeza Rais Mteule wa Kenya Mhe. Uhuru
Kenyatta baada ya jana kutangazwa mshindi wa nafasi ya Urais na Tume
Huru Ya Uchaguzi Kenya ( IEBC).
Tume
Huru ya Uchaguzi Kenya ilitangaza Kenyatta kuwa mshindi kwa kupata kura
8,203,290 (54.27%) dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga 6,762,224
(44.74%), kufuatia matokeo hayo Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli
ametoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine
tena.
"Nakupongeza Ndg.Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Kenya kwa kipindi kingine. Nakutakia mafanikio mema" alisema Rais Magufuli kupitia mtandao wake wa Twitter
Kwa
mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi Kenya (IEBC) ilisema kuwa uchaguzi huo
ulikuwa wa huru na haki na kudai kuwa umekuwa ni uchaguzi wa kipekee kwa
Kenya kwani watu waliojitokeza kujiandikisha na kupiga kura ni wengi
zaidi ukilinganisha na chaguzi zilizofanyika kipindi cha nyuma.
SHARE
No comments:
Post a Comment