Mwenyekiti
wa Bodi ya Msamaha kwa Wafungwa (Parole), Augustine Mrema ametoa
shukrani zake kwa Rais John Magufuli kwa kumsaidia kupata matibabu
nchini India na kufanikiwa kupona ugonjwa wa kansa.
Mrema
alisema kwa sasa utendaji wake wa kazi utaimarika kwa kuwa ameshapona
ugonjwa uliokuwa ukimsumbua na kushindwa kutumikia wananchi na Taifa.
Akizungumza
mbele ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama
Mwokozi jijini Dar es Salaam, alisema kuanzia sasa atamsaidia vizuri
Rais katika nafasi yake ya kuwatetea wafungwa kupitia msamaha wa Bodi ya
Parole.
Alisema amefikia hatua ya kutoa shukrani kwa sababu ya muujiza aliopata kutoka kwa viongozi wa Serikali na dini waliomuombea.
Paroko
Kiongozi wa kanisa hilo, Cathbert Magaga aliwataka waumini wengine
kuiga mfano wa Mrema wa kutoa shukrani na siyo kunyamaza kwa kuwa Mungu
atawasaidia.
SHARE
No comments:
Post a Comment