TRA

TRA

Saturday, August 12, 2017

Mtu mzee zaidi duniani afariki akiwa na miaka 113

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mtu aliyetambuliwa rasmi kuwa mzee zaidi duniani ambaye ndiye pekee aliyesalia katika familia yake baada ya mauaji ya halaiki ya Wayahudi amefariki akiwa na umri wa miaka 113.

Yisrael Kristal ambaye ni mzaliwa wa taifa la Poland alifariki siku ya Ijumaa mwezi mmoja kabla yake kutimiza umri wa miaka 114, chombo cha habari cha Israel kimeripoti.


Bwana Kristal aliyeishi mjini Haifa, Israel aligonga vichwa va habari mwaka uliopita baada ya kuamua kusherehekea utamaduni wa mvulana aliyefikisha umri wa miaka 13, ambao hufahamika kama mitzvah, akiwa amechelewa kwa karne moja.
Sherehe hiyo haikufanyika alipotimiza miaka 13 mwenyewe kwa sababu vita vya dunia vya kwanza vilikuwa vimeanza.

Bwana Kristal ni mzaliwa wa kiji cha Zarnow, takriban kilomita 146 kusini magharibi mwa Warsaw 1903.

Akiwa mwana wa msomi wa kidini, Bwana Kristal alimpoteza mamake na babake wakati wa vita vya dunia vya kwanza kulingana na ripoti.

Baadaye alielekea Lodz kufanya kazi ya bishara ya familia.
Baada ya uvamizi wa Poland uliotekelezwa na Wajerumani wa Nazi 1939, bwana Kristal na familia yake walipelekwa katika nyumba za Lodz.

Watoto wake wawili walifariki na Kristal na mkewe Chaja feige Frucht walitumwa Auschwitz 1994 baada ya mtaa huo kufungwa.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger