Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.
Mwanamume mmoja
mweusi ambaye anadaiwa kulazimishwa kuingia ndani ya jeneza na wanaume
wawili wazungu ambao walitisha kumchoma akiwa hai ametoa ushahidi mbele
ya mahakama nchini Afrika Kusini.
Mahakama ilicheza video ya kisa hicho ambapo bwana Mlotshwa anaweza kusokika akilia na kuomba washambuliaji kumsamehe.
Anadai kuwa wakulima Theo Jackson na Willem Oosthuizen walimfunga kwa nyaya wakampiga na kutishia kumpiga risasi.
Washukiwa hao wawili wanakana hilo wakidai kuwa walimpata bwana Mlotswa akiiba nyaya.
Wanasema kuwa lengi lao lilikuwa ni la kumfunza adabu. Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment