NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAFANYAKAZI
wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel-Tanzania, wamehimizwa kuzingatia
utendaji wa kazi wenye malengo na kutimiza malengo hayo bila kukata tama.
Hayo
yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw.Anjay
Rughani, (pichani), wakati akitoa mada kwenye semina ya kuhamasisha (motivation),
wafanyakazi hao, makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo Agosti
23, 2018.
“Mimi
ni Mtanzania kutoka Mbeya, nimepitia mikiki mikiki mingi hadi kufikia hapa
nilipo, na ningewaomba ndugu zangu, kila uamkapo fanya tathmini ya malengo
uliyojiwekea ni kwa kiasi gani umefikia tena bila kuchoka” Alisema.
Bw.Rughani
ni mmoja kati ya watanzania wawili ambao wanashika wadhifa mkubwa, (CEO),
kwenye taasisi kubwa ya kifedha yenye nguvu kama Standard Chartered Bank.
Mtanzania mwingine ni Dkt. Charles Kimei, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, benki ambayo chini ya uongozi wake, imepiga hatua kubwa miongoni
mwa taasisi kubwa za kifedha hapa nchini.
Hata
ninyi hapa leo mnaweza kufikia hatua ambayo mimi nimefikia, kwani hakuna jambo
linaloshindikana, muhimu ni kuweka malengo, kujielekeza kwenye malengo hayo na
kujituma kwa kiwango cha juu na hatimaye utaona matokeo bora, alisisitiza.
Lengo
la semina hii ni kuhamasisha wafanyakazi wa kampuni ya Airtel, kuzingatia
misingi ya utendaji kazi, kwa kujituma, ubunifu, kuweka malengo na kuyatekeleza
hadi kuona matokeo yake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Airtel-Tanzania Bw. Sunil
Colaso, akliwaambia wafanyakazi hao wakati akimkaribisha Bw. Sunil kutoa “somo”
hilo.
![]() |
|
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kushoto),
akimpongeza Bw. Rughani, baada ya kuwasilisha mada hiyo.
|
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo.
Mfanyakazi wa Airtel- Tanzania, akizungumza wakati wa semina hiyo.
Mfanyakazi wa Airtel- Tanzania, akizungumza wakati wa semina hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kushoto),
akibadilishana mawazo na Wakurugenzi kutoka kulia ni Isack Nchunda(Mkurugenzi
wa Masoko, Frank Filman (Mkurugenzi wa IT), na Emmanuel Luanda, (Kaimu Mkurugenzi
wa Mtandao-Network)
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
Airtel-Tanzania, Bw. Sunil Colaso, (kulia), akizungumza jambo na Afisa Mtendaji
Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani
Baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria semina hiyo.
Wafnyakazi wakisikiliza kwa makini "somo" lililokuwa likitolewa na Bw. Rughani.
Bw. Sanjay Rughani, na Bw. Sunil Colaso, wakiwa katika picha ya pamoja na watayarishaji w semina hiyo.
Afisa
Mtendaji Mkuu, wa Standard Chartered Bank-Tanzania, Bw. Anjay Rughani, ambaye
ni mmoja kati wa watanzania wachache wanaoshikilia nafasi hiyo ya juu kwenye
taasisi za kimataifa, akizungumza wakati wa semina ya kuwahamasisha
(motivation), wafanyakazi wa kampuni ya simu za mikononi, Airtel, makao makuu,
jijini Dar es Salaam, Agosti 23, 2017.
Wafanyakazi wakisikiliza
SHARE






















No comments:
Post a Comment