Kamari
iliyochezwa katika Casino kubwa ya Las Vegas mwishoni mwa wiki imevunja
rekodi na kuwa kubwa kiasi cha mifumo ya kuchezea kamari ya ‘sportsbook’
kushindwa kuhimili.
Kwa
mujibu wa Espn, mtu mmoja ambaye ‘alibet’ mwishoni mwa wiki aliweka
historia kwa kuweka dau la dola za Kimarekani laki nane na themanini
elfu ($880,000) akisimamia kuwa Mayweather atampiga McGregor katika
pambano lao litakalofanyika Agosti 26 mwaka huu katika ukumbi wa
T-Mobile Arena nchini Marekani.
Hiki ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kuwekwa kwenye kamali kwa mkupuo katika historia ya michezo ya masumbwi.
Kwa
mujibu wa ‘bet’ hiyo, kama Mayweather atampiga McGregor, mtu huyo
‘aliyebet’ atajipatia faida ya dola za Kimarekani laki moja na sitini
elfu ($160,000).
Dau hilo
la kamali liliripotiwa kwa mara ya kwanza na Vegas Stats &
Information, ambayo ilituma picha ya tiketi yake kwenye mitandao ya
kijamii.
Hata
hivyo, tiketi hiyo ilionesha kwa makosa kuwa mcheza kamali angepata
faida ya $120,000 badala ya kiasi sahihi cha $160,000, kutoka na mfumo
kushindwa kuhimili tarakimu hizo kwani mfumo hauruhusu kutoa jumla ya
zaidi ya dola milioni moja, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ‘Sportsbook’,
Chris Andrew. Hii ina maanisha $880,000 + $120,000 ndio mwisho wa
tarakimu zinazokubalika kwenye mfumo huo.
Andrews
amesema kwa namna ambavyo mfumo huo ulivyo, malipo yanayompa nafasi
Mayweather yanapaswa kuwa dola za Kimarekani milioni moja ($1.04
million).
SHARE
No comments:
Post a Comment