![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5MpdHk_t5NOqh2p50jSadP7WuB9E7SV0XYpLiANyeKoQmREN8EznO2M9ItYLQbIRmreMG3mjEyjsaEyJli1Okicmhvy3B0By3mquW2xBIC9NyQTBL7Wv15r3HQuepIbY7K8cipNkk30E/s640/wabunge%252Bcuf.jpg)
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017
imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliofutwa
uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba
ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge hadi hapo kesi ya msingi itakapomalizika.
Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia
mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa
mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao rukhsa kuapishwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment