August 4, 2017 Mfanyabiashara Yusuf Manji anayekabiliwa na tuhuma za
kesi ya uhujumu uchumi ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kwa sababu ana kesi nyingine Mahakama Kuu.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya
Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi, kueleza kesi imeitishwa kwa
ajili ya kutajwa, na upelelezi wa kesi haujakamilika lakini Mshtakiwa wa
kwanza ambaye ni Manji ameshindwa kwa sababu ana kesi nyingine Mahakama
Kuu.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi
Agosti 9, 2017 kwa ajili ya kutajwa ingawa washtakiwa wenzake ambao ni
Deogratias Kisinda, Abdallah Sangey na Thobias Fwele wamefika mahakamani.
SHARE
No comments:
Post a Comment