Pam D na Christian Bella.
MSANII wa
Bongo Fleva, Pamela Daffa ‘Pam D’ amefunguka kuwa, ukaribu alionao na
staa wa Muziki wa Dansi, Christian Bella ‘Obama’ umembeba kwa kiasi
kikubwa.Akistorisha
na Over Ze Weekend, Pam D anayebamba na Wimbo wa Ngoma Droo akiwa
amemshirikisha Bella, alisema tangu kutoka kwa wimbo huo amekuwa
akizunguka na Bella sehemu nyingi kwa ajili ya kuutambulisha japokuwa
amekuwa akikutana na changamoto za hapa na pale za kuhisiwa huenda
wameanzisha uhusiano.
“Liko
wazi, Bella amenibeba sana, nashukuru kwa hilo. Wapo wanaohisi tofauti
baada ya kutoa wimbo huu kwa sababu nakuwa naye karibu kote
anapokwenda,” alisema Pam D.
SHARE
No comments:
Post a Comment