Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Leo ameendelea na ziara yake
mkoani Katavi, akiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kukagua huduma za
Afya zitolewazo nchini.
Katika ziara hiyo Waziri huyo
ametembelea kituo cha Afya Nsimbo na Inyonga katika Halmashauri ya
Mlele na Usevya Halmashauri ya Mpimbwe.
Akiwa katika vituo hivyo Waziri
huyo alifanya ukaguzi kwenye maendeo mbalimbali ya utoaji
huduma,upatikanaji was Dawa na vifaa Tina,miundombinu ya vituo hivyo
pamoja na kuongea na watumishi wa Afya kujua changamoto zinazowakabili
na kufanyia ufumbuzi ili kuleta ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Aidha,akizungumza na watumishi
hao,Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha kuwa
dawa zinawafikia wananchi katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Waziri huyo amekua akisisitiza
Mara kwa Mara katika ziara zake suala ya usimamizi wa Dawa na vifaa Tiba
kwenye hospitali na vituo vya Afya nchini ili kuondoa malalamiko mengi
toka wa wananchi wanaofika kupatiwa huduma.
Leo Waziri ataendelea na ziara take Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa
SHARE
No comments:
Post a Comment