Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William
Ntinika (kushoto), akionyesha nembo mpya ya Klabu ya Biashara ya NBC
mara baada ya uzinduzi rasmi wa klabu hiyo mjini Mbeya hivi karibuni.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa
waandamizi wa serikali mkoani humo. Wanaoangalia nyuma yake ni Ezekiel
Mwakibinga, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Essau
Kamwela.
Mwakilishi kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Gabriel Mwangosi (kulia), akifundisha masuala
mbalimbali kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na NBC
kwa wateja wake wadogo na wa kati mjini Mbeya. Semina hiyo ilifuatiwa na
uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani Mbeya hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, William
Ntinika (kushoto), akikaribishwa na Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Alvis
Ndunguru wakati akiwasili kwa ajili ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara
ya NBC mkoani Mbeya. Katikati ni Meneja Mahusiano wa NBC, William
Kallaghe. Uzinduzi huo ulitanguliwa na semina ya siku moja juu ya
kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.
Mkurugenzi wa
Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Klabu ya Biashara ya NBC, mkoani Mbeya. Uzinduzi huo
ulitanguliwa na semina ya siku moja juu ya kuwajengea uwezo
wafanyabiasha wadogo na wa kati. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wateja wa
NBC, wajasiriamali na maofisa wa serikali mkoani humo.
Baadhi ya
wateja wa NBC mkoani Mbeya wakijipiga picha wenyewe ‘maaarufu kama
selfie’ wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC mkoani
humo hivi karibuni. Uzinduzi huo ulitanguliwa na semina ya siku
moja juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati
ilihudhuriwa na wateja wa NBC, wajasiriamali na maofisa waandamizi wa
serikali mkoani humo.
SHARE
No comments:
Post a Comment