Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya
Utalii Tanzania, Bi Devota Mdachi amemkabidhi Mwanamitindo Joctan Makeke
bendera ya Tanzania ili aweze kuipeperusha katika jukwaa la mashindano
ya “Face of Culture” yanayotarajiwa kufanyika Septemba 9, 2017 nchini
Nigeria. Katika Mashindano hayo yatakayohusisha makundi mbalimbali,
Joctan ambaye ni mwanamitindo pekee aliyepata nafasi ya kuiwakilisha
Tanzania katika kundi la mavazi ya kiutamaduni.
Wakati wa makabidhiano hayo, Bodi
pia imempatia mwanamitindo huyo vipeperushi vinavyotangaza Utalii wa
Tanzania kwa lengo la kuwahamasisha washiriki wengine Kutoka nchi
mbalimbali kuja kuvitembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment