ALIYEKUWA
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania, (ATC), Bw. David Mataka na
mwenzake mmoja wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela au kulipa faini ya
shilingi Milioni 35 kila mmoja.
Uamuzi
huo umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
Septemba 13, 2017 ambapo mwenzake ni aliyekuwa Afisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha cha
ATCL, Bw.Elisaph Mathew.
Mahakama
hiyo pia imemuachia huru aliyekuwa Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za ndani (Internal
auditor) wa ATCL, Bw.Wiliam Haji.
SHARE
No comments:
Post a Comment