HALMASHAURI ya
Manispaa ya Ilala imesema vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto
chini ya miaka 18 vimepungua kutoka kesi 199 zilizoripotiwa kwenye
vituo vya polisi kwa mwaka 2016 hadi kesi 109 ziliropitiwa kwenye vituo
hivyo kwa mwaka 2017.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ofisa Mkuu wa Idara ya
Jamii na Ustawi wa Jamii na Vijana wa Manispa hiyo Francisca Makole
akitoa taarifa ya mwaka ya maendeleo ya ukatili katika halmashauri ya
wilaya ya Ilala, amesema vitendo hivyo vimepungua kutokana na elimu
wanayotoa kwa jamii.
Amesema kutokana
na elimu hiyo kumekuwa na ushirikiano unaotolewa na jamii hususani
katika kuripoti matukikio hayo ya ukatili kwa watoto kwenye mamlaka
husika. Alibainisha pia ukatili wa kingono umepungua kutoka asilimia
32 kwa mwaka jana hadi kufikia asilimia 19 kwa mwaka huu.
“Sahivi watu
wamekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa pindi mtu anapofanyiwa ukatili
wowote katika jamii,hususani kutoa taarifa kwenye kituo cha mkono kwa
mkono ambacho kinatumika kutoa huduma ya kupinga ukatili wa kijinsia,hii
imechangia kupungua kwa vitendo vya ukatili’’ amesema Makole.
Makale amesema
kwa sasa wamekuwa wakishirikiana na watu mbali mbali ambao wanajitolea
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuweza kutokomeza vitendo
vya ukatili wa kijinsia ndani ya manispaa hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment