Mechi
ya kufuzu Michuano ya kombe la dunia kati ya Afrika Kusini na Senegal
itarudiwa tena baada ya refa aliyesimamiwa mechi hiyo kupigwa marufuku
na Fifa.
Refa huyo raia wa Ghana Joseph
Lamptey, alipiwa marufuku kwa kusimia mechi kwa njia isiyofaa alikutwa
na kosa la kuwapa penalti Afrika Kusini ambao walishinda kwa mabao 2-1
mwezi Novemba mwaka uliopita kwa kunawa mpira lakini kanda ya video
baaadaye ilionyeha kuwa mpira huo ulimgonga kwenye goti mlinzi wa
Senegal Kalidou Koulibaly.
Mechi hiyo itachezwa tena Novemba
mwaka huu,Lamptey alipigwa marufuku ya maisha mwezi Machi lakini jana
Jumatano marufuku hiyo ilibatiliswa na mahakama ya michezo.
Lamptey, ambaye pia alisimamia
mechi katika mashindano ya Olimpki huko Rio mwaka uliopita alikataa na
kungea na BBC baada ya kupigwa marufuku ambayo ilikuja baada ya Senegal
kulalamika.
Senegal na Afrika Kusini kwa saa wako nafasi ya tatu na nne mtawalia katika kundi la la D nyuma ya Burkina Faso na Cape Verde.
Ni timu moja pekee ya kwanza katika kundi ambayo itafuzua kwa mechi za kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.
SHARE
No comments:
Post a Comment