Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi
wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua
kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka
watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa
wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao
cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za
kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa
uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na
almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge
kwanza.
Chanzo: Mwananchi
SHARE
No comments:
Post a Comment