Fifa wamelikataa
ombi la Leicester City la kutaka kumsajili kiungo wa kati Adrien Silva
baada ya klabu hiyo kuchelewa kwa sekunde 14 kumaliza usajili wake kabla
ya muda wa mwisho kufika.
Adrien Silva amefungia Urengo bao moja katika mechi 20
Usajili wa Silva kama mchezaji wa klabu hiyo katika shirikisho hilo linalosimamia soka duniani haukukamilishwa kwa wakati.
Hii ina maana kwamba mchezaji huyo ni wao lakini hawezi kuwachezea hadi dirisha lifunguliwe tena Januari.
Leicester wameanza mchakato wa kukata rufaa uamuzi huo wa Fifa.
Msemaji wao amesema: "Tunafanya juhudi za Adrien na Sporting Clube de Portugal kutatua matatizo kuhusu usajili wa mchezaji huyo na tunajaribu kutafuta suluhu."
Klabu hiyo inammiliki Silva lakini kuna baadhi ya sehemu za mkataba ambazo hazikuwa zimekamailishwa kikamilifu.
Hii ina maana kwamba watahitajika kulipa ujira wake hadi wajaribu kukamilisha usajili wake kikamilifu Januari.
Silva, 28, ni mzaliwa wa Ufaransa na alikuwa kwenye akademi ya klabu ya Sporting.
Alicheza kwa mkopo Maccabi Haifa na Academica.
Amechezea Ureno mechi 20 za kimataifa na kuwafungia bao moja na aliwachezea waliposhinda Euro 2016.
Leicester pia walimuuza kiungo wa kati Danny Drinkwater kwa Chelsea kwa £35m dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa soko Alhamisi wiki iliyopita.
SHARE









No comments:
Post a Comment