![](https://matukiotz.co.tz/wp-content/uploads/2017/09/MAGUFULI.jpg)
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaama wakati akimuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma na kusema anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni wengi sasa ila anaomba asipewe hiyo orodha.
Sisi wanasiasa tunaogopa kunyonga, natambua kuwa sasa orodha ya watu ambao wanatakiwa kunyongwa ni kubwa sana ila mimi naomba hiyo orodha msiniletee kwa sababu najua ugumu wake ulivyo” alisisitiza Rais Magufuli Mbali na hilo Rais Magufuli amesema kuwa amechukua muda mrefu kumteua
Jaji Mkuu wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba alikuwa anatafuta mtu ambaye anaweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa hivyo alipojilidhisha na jaji huyo ndiyo maana ameamua kumteua kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment