Mfanyabiashara Yusuf Manji, akiwa huru
wakati anatoka mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,
Septemba 14, 2017.
NA
K-VIS BLOG
OFISI ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, (DPP), imeiambia Mahakama ya
Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam kuwa haina nia ya kuendelea na Kesi
ya Uhujumu Uchumi iliyomfungulia Mfanyabiashara maarufu nchini, Bw. Yusuf Manji
na kwa maana hiyo Mahakama ikaamua kuifuta kesi hiyo na kumuachia huru
Mfanyabiashara huyo.
Pamoja na Manji, pia washtakwia wenzake wawili, nao wameachiliwa huru.
Mkurugenzi wa ashtaka aliwasilisha hati ya kuomba kuondolewa kwa
mashitaka dhidi yao kwa kuwa hana nia ya kuendelea kuwashitaki.
Baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, kueleza nia
hiyo ya DPP, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bw. Huruma Shaidi, aliyekuwa
akisikiliza shauri hilo aliliondoa na kuwaachia huru washitakiwa hao.
Baada ya kusota rumande kwa miezi kadhaa, leo hii Manji amepata fursa ya
kuungana na familia yake na jamaa zake na kabla ya kuachiwa huru, Manji na
wenzake waliletwa Mahakamani hapo wakitokea Mahabusu ya gereza la Keko.
Manji
alishtakiwa kwa kosa la uhujumu uchumi baada ya kukutwa na vitambaa vya sare za
jeshi vyenye thamani ya shilingi milioni 200 pamoaja na mihuri ya jeshi.
“Kama
tulivyomzoea Yusuf Manji, ni mfanyabiashara na atarudi na kusimamia shughuli
zake za kila siku, uhuru wake ni muhuimu na tunaimani atanednelea na biashara
zake.” Alisema wakili wake, Bw. Hudson Ndusyepo.
Mfanyabiashara
huyo bado anakabiliwa na kesi nyingine ya matumizi ya madawa ya kulevya ambapo
kesi hyo imefikia hatua ya utetezi.
Manji akiwa na wakili wake Bw.Hudson Ndusyepo.
SHARE
No comments:
Post a Comment