Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai
(kulia) baada ya kuzindua Awamu ya Pili ya
Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma Septemba 14, 2017. Kushoto ni Balozi wa Ireland Nchini, Paul
Sherlock.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ireland Nchini, Mhe. Paul
Sherlock (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini, Bw. David
Omozuafoh (kulia) baada ya kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa
Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Septemba 14, 2017.
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akizindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo
Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14,
2017. Kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri
Mkuu, Kasim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Awamu ya Pili ya
Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge
mjini Dodoma Septemba 14, 2017.Kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
NA OWM,
DODOMA
WAZIRI Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa amesema Mataifa ya Afrika
yanatakiwa yaandae maarifa, vitendea kazi na rasilimali watu watakaoweza
kusimamia na kuendeleza ipasavyo sekta ya madini na kuleta tija kwa Taifa
husika na wananchi kwa ujumla.
Amesema taarifa za kijiolojia zinaonesha kuwa Afrika ni Bara
lenye utajiri mkubwa wa rasilimali madini huku sehemu kubwa ya madini hayo
yakiwa bado hayajaanza au yako kwenye hatua mbalimbali za uendelezaji.
Ametoa kauli hiyo (Alhamisi, Septemba 14, 2017) alipofungua
mkutano wa 37 wa Baraza la Uongozi wa Kituo cha Madini na Jiosayansi cha Afrika
(AMGC) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo hicho mkoani Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu amesema rasilimali za madini ilizopo Barani Afrika
inaweza kuwa ni chanzo kikubwa cha kusukuma maendeleo ya kiuchumi na kijamii
katika nchi nyingi iwapo itasimamiwa vizuri.
Ametolea mfano Tanzania ambayo licha ya kuwa na utajiri mkubwa
wa madini ya dhahabu, almasi, chuma, madini ya vito kama tanzanite lakini
mchango wa sekta ya madini ni asilimia 4.8 ya pato ghafi la Taifa.
“Changamoto kuu kwa sasa ni kwa jinsi gani tunaweza kuwa na
sekta ya madini inayotoa mchango stahiki katika nchi husika pamoja na kusimamia
sekta hii kwa kuwafanya wananchi wetu hususan katika maeneo yenye rasilimali
wakanufaika na kuona fahari badala ya kuacha mashimo, umasikini na mateso kwa
wananchi.”
Amesema lengo la kuanzishwa kwa kituo hicho ambacho leo
kimetimiza miaka 40 ni kuhakikisha sekta ya madini inawajibika kuleta maendeleo
ya kijamii na uchumi pia ikijali masuala ya mazingira, hivyo ni vema kikatumika
kama ilivyokusudiwa.
Waziri Mkuu amesema kituo hicho kikitumika vema kwa mujibu wa
kusudia la uanzishwaji wake kinaweza kuleta tija kubwa kwenye sekta ya
uchumbaji wa madini, uongezaji wa thamani na usimamizi wa sekta.
Amesema kituo hicho ni moja kati ya taasisi chache duniani yenye
teknolojia za kisasa ambazo zinaweza kusaidia kufanya uchambuzi wa miamba na
madini yaliyimo. “Pia ni sehemu ambayo unaweza kupata huduma za ushauri na
kusaidia teknolojia utakayoweza kutumia ili kufanya uzalishaji wa madini
mbalimbali.”
Hivyo amewakumbusha wajumbe na wanachama wa AMGC kuwa kituo
hicho hawajakitumia ipasavyo ni vema kikatumika ili kupata tija kwenye
uendelezaji na usimamizi wa madini, ambapo ameiagiza Bodi iandae mpango
utakaoziwezesha nchi wasnachama kukitumia.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani amesema kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali ya kwanza ni kwa wanachama kutolipa ada kwa wakati.
Dkt. Kalemani ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Kituo
cha AMGC amesema changamoto ya pili ni wanachama wa kituo hicho kutokitafutia
wateja na masoko. Pia miundombinu mingi ya kutuo ni chakavu.
Akizungumzia changamoto hizo Waziri Mkuu ameziagiza nchi zote
zinazodaiwa ada ikiwemo Tanzania zilipe ada stahiki kwa wakati na kuweka
mkakati wa kukitangaza kituo hicho ili kukiwezesha kupata wateja kwa ajili ya
kutumia huduma zitolewazo.
Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson akitoa maelezo kabla ya Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa Kuzindua Awamu ya Pili ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa
Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia kwake ) wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi walioshiriki katika Awamu ya Pili
ya Mradi wa Kuujengea Uwezo Mhimili wa Bunge (LSP- 11) kwenye ukumbi wa
Bunge mjini Dodoma Septemba 14, 2017.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
SHARE
No comments:
Post a Comment