"Migogoro mingi ya Ardhi ni kutokujituma kwa watu wetu" RC Gambo
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati
anahitimisha mkutano wake na wananchi wa wilaya ya Karatu wenye kero
mbalimbali za Ardhi,Nyumba na Makazi.
"Toka
nianze mikutano mikutano hii na wakazi wa Jiji la Arusha na leo nipo
hapa Karatu migogoro mingi si mikubwa kama inavyoonekana bali
inachangiwa na uzembe wa watu wetu katika mabaraza ya Ardhi na mahakama
kutokutimiza wajibu wao ipasavyo" alisema Gambo.
Katika
mikutano hiyo maalum ambayo mkuu huyo wa mkoa ameshaifanya katika jiji
la Arusha na Karatu amekutana na migogoro mingi ambayo kiuhalisia
imeshasuluhishwa katika hatua mbalimbali za kimaamuzi lakini wananchi
hao hawajapewa mrejesho.
"Tatizo
letu sisi watendaji ni kutokuwaandikia watu hawa wa nini tumekifanya
katika maamuzi yetu na kutokuweka kumbukumbu sahihi, kama mmeshughulikia
tatizo la mtu mpeni mrejesho kwa maandishi na kama ataona hajaridhika
mshaurini hatua zaidi za kufuata na jambo hilo liwekwe kwenye kumbukumbu
zetu ili akija wakati mwingine tusipate shida kwa kudhani ni jambo
jipya" alisisitiza Mhe Gambo.
Vilevile
amemuagiza Kamishna wa Ardhi kutuma timu maalum itakayoshughulikia kero
hizo ndani ya muda mfupi na kuyafanyia ukaguzi mabaraza yote ya Ardhi
wilaya za Arusha mjini na Kararu.
"Kamishna
nitakutana mara baada ya ziara ya mwenge kupita mkoani mwetu ulete timu
maalum itakayopiga kambi hapa kumaliza kero hizi kwani hapa kuna
wengine wala hawana migogoro ya ardhi bali wamevamiwa kwenye maeneo yao
watu kama hawa polisi ndio sehemu husika na sio kwenye mabaraza ya
ardhi, vilevile ukayafanyie ukaguzi mabaraza ya Ardhi ya Arusha mjini na
Karatu kwani nayo sioni kama wanafanya kazi zao sahihi sana" aliagiza
mkuu huyo wa mkoa.
Katika
mikutano hiyo maalum aliyoianza tarehe 29/08/2017 kwa Jiji la Arusha na
tarehe 30/08/2017 kwa wilaya ya Karatu Mkuu huyo wa mkoa ameambatana na
wataalam wa Ardhi toka ofisi ya Kamishna wa Ardhi,Msajili wa hati
Kanda, wataalam wa Ardhi mkoa wa Arusha, mwanasheria toka ofisi ya
mwanasheria mkuu wa serikali na wataalam mbalimbali toka halmashauri
husika.
Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kua na migogoro mingi ya Ardhi na ya muda mrefu.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(katikati) akiendesha mkutano wa
kuwasikiliza wanachi wa Jiji la Arusha kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Arusha Mjini, Fabian Daqqaro na kulia ni Kaimu katibu Tawala Mkoa wa
Arusha Bwana. Chitukuro .
Wananchi wa wilaya ya Karatu wakiwa katika makundi kusubiri kuonana na RC Gambo na kutoa malamimiko yao.
SHARE
No comments:
Post a Comment