Na. Hassan Mabuye
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt
Angeline Mabulla amezionya halmashauri nchini ambazo zinaomba kujengewa
Nyumba na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na baada ya Shirika
kuwajengea wanazitelekeza.
Mhe Mabulla ameyasema
hayo wakati alipofanya ziara Mkoani Shinyanga na kugundua kati ya nyumba
50 zilizojengwa na NHC kwa ajili ya Halmashauri Kahama ni nyumba 1 tu
ambayo imenunuliwa, licha ya kuwa halmashauri hiyo ndio iliomba kuje
gewa nyumba hizo.
Huwezi kuomba kitu
halafu kwenye kukichukua iwe ni ugomvi, kwa hiyo sasaivi naielekeza
Shilika la Nyumba la Taifa hakuna kujenga nyumba mpya mahala popote kama
huna makubaliano ya wali na Halmashauri husika. Amesema Mhe. Mabulla
Katika hatua Nyingine
Naibu Waziri huyo ameendelea kuwabana maafisa wa ardhi ambao hawasimamii
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ipasavyo na kuto kuwashughulikia.
Mabulla aliwataka
maafisa adhi wa halmashauri ya Shinyanga kumpatia majina ya wadaiwa sugu
100 wa awali ambao hawajalipa kodi ya pango la ardhi kwa miaka mitano
iliyopita ili wafikishwe mahakamani au mali zao kupigwa mnada.
Nae Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bibi Zainab Tellack ametumia nafasi hii kumuomba Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabulla
kumsaidia kutatua baadhi ya migogoro inayoukabili mkoa wa Shinyanga
kabla ya kuondoka.
Katika kusimamia hilo
Mhe. Mabulla alitembelea masijala ya ardhi ambayo hutumika kuhifadhia
kumbukumbu na nyaraka za zinazohusu hatimiliki na kumuagiza Kamishna
Msaidizi wa Ardhi kanda ya Magharibi kuwaelekeza jinsi ya kutunza
kumbukumbu maafisa wa ardhi wa halmashauri ya Shinyanga ili kuepuka
migogoro.
SHARE
No comments:
Post a Comment