Afisa
Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt. Laurent Shirima, (kulia), akibadilishana
hati na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),
Bi. Beng’i Issa, baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano
baina ya taasisi hizo mbili utakaodumu kwa miaka mitanmo. Mkataba huo
mumesainiwa jijini Dar es Salaam Septemba 14, 2017. (PICHA NA EMMANUEL MASAKA WA BLOGU YA JAMII)
MAMLAKA
ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), wametiliana saini mkataba wa miaka mitano
wa ushirikiano
Mkataba
huo uliosainiwa leo Septemba 14, 2017 jijini Dar es Salaam, utawezesha PPRA na
NEEC kushirikiana kiutendaji ili kuwawezesha wajasiriamali
wadogo na wa kati kushiriki kwenye
fursa mbalimbali zinazopatikana katika manunuzi ya umma.
Akizungumza
wakati wa hafla ya utilianaji saini mkataba huo, Afisa Mtendaji
Mkuu wa PPRA Dk. Laurent Shirima, lengo linguine ni mamlaka
kuhakikisha kigezo mojawapo wakati wa hatua ya tathimini
kwenye zabuni za umma cha upendeleo kwa ajasiriamali wadogo
na kati kinazigatiwa.
“Pia
kila mwaka PPRA na NEEC kufanya tathimini ya pamoja ili kujua namna
taasisi nunuzi zinavyotekeleza au kuzingatia ushiriki wa wajasiriamali
wadogo na wakati,”alisema Dk. Shirima.
Malengo
mengine ni PPRA na NEEC kufanya tafiti za pamoja zitakazo jikita
zaidi katika uwezeshaji na ushiriki wa wajasiriamali wadogo
na kati kwenye michakato ya manunuzi ya umma.
“Suala
la kuwajengea wananchi uwezo wa kupambana na umasikini kwa kushiriki
katika shughuli za kiuchumi limekuwa kipaumbele kikubwa cha
serikali na hasa ya awamu ya tano.
Ili
kufanikisha azma hiyo , serikali imekuwa ikiandaa sera na sheria mbalimbali
zinazoweka mazingira mazuri ya wananchi kushiriki na kuitumia
fursa za kibiashara,”lifafanua Dk. Shirima.
Alisema
moja ya sekta inayotoa fursa kwa wananchi kushiriki kwenye
shughuli za kukuza uchumi wan chi ni sekta ya manunuzi ya umma,
hivyo wananchi mmojammoja au kwa makundi wakijengewa uwezo wanaweza
kuchangamkia fursa zilizopo kwenye sekta hiyo ikiwa ni
pamoja na kushuriki kwenye hatua mbalimbali ya zabuni zinazotolewa
na taasisi za umma.
“Ni
matuani yetu kwamba wananchi walio katika makundi husika
watachangamkia fursa hii ya kujwakwamua kiuchumi na kijamii katika
maeneo yao,”alibainisha.
Alisema
taasisi za ununuzi, hasa halmshauri zinatarajiwa kutekeleza wajibu
wao kwa mujibu wa sheria ili kufanikisha lengo la serikali la kutoa
upendelea kwa makundi maalum yamekuwa yanashindwa kunufaika na
fursa zilizo katika sekta ya ununuzi wa umma.
Kwa
upande wa Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’I Issa, alisema
kupitia ushirikiano huo watahakikisha tathimini ya ushiriki
wa biashara ndogo na za kati unafanyika katika ukaguzi wa
ununuzi wa taasisi za umma.
“Pia
taasisi ambazo zitatoa zabuni kwa wafanyabiashara wadogo na wakati
kwa kiwango kilichoainishwa katika sheria kwa makundi
maalum ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kutambuliwa,”alisema
Beng’i.
Alisema
utekelezaji wa ushirikiano huo unalenga kuhakikisha biashara,
kampuni au vikundi vinavyomilikiwa hasa na wanawake , vijana
na watu wenyeulemavu zinapata fursa kushiriki kwenye zabuni
za taasisi za umma.
“Hii
itasaidia kukuza uchumi wao ili kutekeleza ibara ya 57(e)(vi) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM). Pia kuwezesha kutathimini ushiriki
wa biashara ndogo na za kati ili kupata takwimu sahihi zitakazowezesha
serikali kuchukua hatua stahiki za kuwawezesha,”alibainisha.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt. Laurent Shirima,(kulia), pamoja na
Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng’i Issa wakisaini mkataba wa miaka mitano wa
ushirikiano wanaoshuhudia (kulia )ni Mwanasheria Mwandamizi wa
PPRA, Agnes Sayi na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Ushiriki wa Watanzania
katika Uwekezaji, Esther Mmbaga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Dkt. Laurent Shirima, (kulia), akizugumza wakati wa hafla ya utilianaji saini wa mkataba wa miaka mitano wa ushirikiano baina ya PPRA na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Septemba 14, 2017 jijini Dar es Salaam.(kushoto) ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa
SHARE
No comments:
Post a Comment