Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza
hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia
za ngono uliofanywa nchini Uingereza.
Utafiti huo umebaini kwamba wakati wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana
na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi
wao kwa muda mrefu.
Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na
ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya
kufanya tendo la ngono.
Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliyochapishwa na shirika la BMJ Open.
Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.
Mtaalam wa maswala ya ngono Ammanda
Major amesema kuwa kwa binadamu kukosa hamu ya tendo la ngono sio swala
lilisilokuwa la kawaida na kuna sababu nyingi tofauti ambazo wanaume na
wanawake wanahitaji mabadiliko.
''Kwa wengine ni kawaida lakini wengine husababisha machungu mengi'' ,alisema.
Kwa jumla asilimia 15 ya wanaume na
asilimia 34 ya wanawake waliofanyiwa utafiti huo walisema kuwa
walipoteza hamu ya tendo la ngono kwa muda wa miezi mitatu ama hata
zaidi katika mwaka uliopita.
Kwa wanaume, ukosefu huo wa hamu ya
ngono ulikuwa juu miongoni mwa wanaume wa kati ya umri wa miaka 35-44
huku kwa wanawake ukionekana kati ya umri wa miaka 55 na 64.
Chanzo-BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment