Mkurugenzi
wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (Katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Miss Univerese mwaka jana, Jihan Dimachk
(Kulia) na Miss Earth Tanzania, Lilian Loth.
Mkurugenzi
wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua (wanne kutoka
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na warembo, waandaaji na maofisa wa
Basata mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha kujadili mashindano
hayo.
Mkurugenzi
wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano
haya Maria Sarungi Tsehai (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa kikao na
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).Anayesikiliza Mkurugenzi wa Ukuzaji
Sanaa na Masoko wa Basata, Vivian Shalua na Afisa Sanaa, Bona Leon
Masenge.
Na Mwandishi wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (Basata) limeipongeza kampuni ya Compass
Communications Tanzania kwa kufanya mashindano bora ya Miss Universe
hapa nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Basata,
Vivian Shalua wakati wa kufanya tathimini ya mashindano hayo na
mashindano ya urembo kwa ujumla.
Mrembo
Jihan Dimachk alishinda taji la Miss Universe mwaka jana huku Lilian
Loth akishinda nafasi ya pili katika mashindano hayo.
Shalua
alisema Basata wamefarijika sana na jinsi mashindano hayo
yanavyoendeshwa na hakuna malalamiko yoyote kuhusiana na zawadi na
upendeleo.
Alisema
kuwa kutokana na utaratibu mzuri wa mashindano yao, Basata imeridhia
waandaaji wa mashindano hayo, kufanya mashindano ya mwaka huu na vile
vile kuandaa mashindano ya kutimiza miaka 10 tokea kuanzishwa kwa
mashindano hayo mwaka 2007.
“Pamoja
na kuwa na shindano moja kwa kushirikisha warembo wa mikoa tofauti,
bado Basata imefarijika na jinsi mnavyoendesha na utaratibu unaotumia
kuwapata warembo, uendeshaji wa mashindano mpaka kumpata mshindi,”
“Tunajua
kuwa kuna changamoto za wadhamini na kusababisha kufanya mashindano
yenye kalenda fupi na kuondoa mlolongo wa matukio, hatua hii ni bora
zaidi ili kuondoa malalamiko ya zawadi na mambo mengine, huu ni mfano wa
kuigwa,” alisema Shalua.
Mkurugenzi
wa Compass Communications ambaye pia ndiye mwandaaji mkuu wa mashindano
haya Maria Sarungi Tsehai aliishukuru Basata kwa usimamiaji bora wa
mashindano katika sekta ya sanaa nchini na kusema kuwa watajihidi
kuongeza wigo ili kuona warembo wengi zaidi kutoka mikoa tofauti
wanashiriki katika mashindano yao.
Maria
alisema kuwa pamoja na changamoto zote wanazokabiliana nazo, bado
wanahitaji msaada kutoka Basata ili kupata wadhamini na kufikia malengo
yao katika kuendeleza Sanaa hapa nchini.
“Kwa
sasa kuna changamoto kubwa ya wadhamini wa mashindano, kuna haja ya
kupata msaada kutoka Basata ambao ni chombo cha serikali, mnaweza
kutusaidia kupata wadhamini hata kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi
tunatangaza jina la nchi na utalii pia, tunaamini kupitia kwenu,
tunaweza kupata sapoti kubwa kutoka wizara hiyo, Bodi ya Utalii (TTB) na
mamlaka ya zake kama Tanapa,” alisema Maria.
SHARE
No comments:
Post a Comment