Mhandisi
Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita amewataka Viongozi wa
Serikali Wilayani Chato kusimamia na kufuatilia kwa karibu utekelezaji
wa miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo ili thamani ya fedha
zinazotolewa ionekane.
Akizungumza
baada ya kuwasili wilayani Chato kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa
kwake kuwa Mkuu wa Mkoa, amesema kuwa umefika wakati watendaji kuacha
tabia ya kukaa Ofisini bali waende maeneo mbalimbali ya Wilaya ambapo
kunatekelezwa miradi ili kusimamia kwa karibu miradi inayoendelea.
"
Wananchi wanatakiwa kusimamiwa ata kama fedha ni za kwao ili kuweka
miradi katika ubora unaotakiwa"Alisisitiza Lughumbi. Aidha, alimuagiza
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato kuhakikisha wananchi wanakuwa katika
vikundi ili vishiriki katika ujenzi na utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo katika vijiji kwa kuchangia michango midogo midogo kama
vile kutafuta mawe, kokoto, mchanga. Kazi kubwa ya Halmashauri ni
kuhakikisha wahandisi wanasaidia kupeleka michoro na kusimamia ujenzi wa
miradi ya Zahanati na madarasa katika vijiji husika.
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Chato
kufuatilia ujenzi wa Bweni la wanafunzi shule ya Sekondari Jikomboe
ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi milioni 75 ili kujiridhisha kama
fedha hizo zimetumika kama ilivyokusudiwa na kuona kama thamani yake
inaonekana.
Akiwa
Wilayani Chato Mheshimiwa Robert Gabriel ametembelea shule ya Msingi
Chato na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa sita na vyoo, ujenzi wa
Zahanati ya kijiji Mganza, ujenzi wa Bweni shule ya Sekondari Zakia
Meghj pamoja na Ujenzi wa Soko la dagaa Kasenda na kuagiza takukuru
kufika katika miradi hiyo ili kufuatilia matumizi ya fedha katika miradi
ya Zahanati, Bweni na madarasa.
Vilevile
Mkuu wa Mkoa ametembelea ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na
kupongeza jitihada za utekelezaji wa mradi huo zinazoendelea kwa kufikia
asilimia 63. Awali Meneja wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna
Senkuku alimweleza Mkuu wa Mkoa kuwa uwanja huo una Run way ya Kilometa 3
ambapo hadi kukamilika mradi utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 39.
Utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa uwanja wa ndege Chato ukiendelea.
Mhandisi
Robert Gabriel Lughumbi Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na Viongozi
mbalimbali wa Mkoa na Wilaya ya Chato baada ya kuwasili Wilayani
Chato.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Chato pia ni waziri wa Nishati
Mheshimi Dkt Medard Kalemani.
Meneja
wa Tanroads Mkoa wa Geita Mhandisi Haruna Senkuku akifafanua jambo kwa
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Lughumbi wakati wa ukaguzi
wa ujenzi wa Uwanja wa ndege Chato alipotembelea na kujionea ujenzi
katika moja kati ya ziara yake ya kikazi Wilayani Humo.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongoza viongozi katika ukaguzi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo wakati akikagua
maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa ndege Chato.(PICHA NA MAGESA JUMAPILI
AFISA HABARI MKOA WA GEITA)
SHARE
No comments:
Post a Comment